Ruto Asisitiza Serikali Inapambana na Ufisadi

Naibu wa rais William Ruto amesema kuwa serikali imechukuwa mwelekeo ufaao katika vita dhidi ya ufisadi. Akilihutubia taifa katika ukumbi wa National Theatre, Ruto alisema kuwa serikali inazifadhili ipasavyo taasisi huru ili kuhakikisha kuwa kesi zilizosalia za ufisadi zinakamilishwa na mali zilizopatikana kupitia kwa njia za ufisadi zinatwaliwa. Naibu wa rais alisema kuwa serikali inaweza tu kupambana na ufisadi kwa kufuata sheria zilizowekwa kwenye katiba huku akitoa wito kwa taasisi zote huru zilizotwikwa jukumu la kupambana na ufisadi kuhakikisha kuwa kesi zote zilizosalia za ufisadi zinatatuliwa. Naibu rais alisema kuwa miradi mikuu ya kiuchumi ambayo serikali inatekeleza inanuia kuimarisha uchumi wa taifa hili na kubuni nafasi za ajira. A�

A�