Ruto amesema ana imani kwamba Jubilee itashinda Urais kwenye uchaguzi mkuu

Naibu wa Rais William Ruto amesemaA� ana imani kwamba chama cha Jubilee kitashinda Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao wa tarehe nane mwezi agosti mwaka huu.Akiongea katika soko la Kambu lililoko katika eneo bunge la Kibwezi mashariki alikosimama wakati wa ziara yake katika kaunti ya Makueni kuwahimiza watu kujiandikisha kwa wingi kuwa wapiga kura,naibu wa Rais alisema chama cha Jubilee kitajipatia ushindi mkubwa kulingana na takwimu ambazo zimetolewa na tume huru ya uchaguzi na mipaka kuhusu wapiga kura wapya ambao wamesajiliwa kufikia sasa.Ruto alisema chama cha jubilee kimejitolea kuhakikisha serikali inawashirikisha wote na ugavi sawa wa raslimali bila kujali misimamo ya kisiasa. Naibu wa Rais aliihimiza jamii ya wakamba kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kuchaguliwa tena akisema serikali yake haikutenga eneo hilo katika miradi ya maendeleo na uteuzi wa nyadhifaa kuu serikalini.Seneta wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko alisema ni jambo la kusikitisha kuiona jamii ya Kamba ikipotoshwa kujiunga na upinzani ilhali ina nafasi nzuri serikalini.Alimhimiza kinara mwenza wa Cord kalonzo Musyoka ajiunge na chama cha Jubilee kwasababu chama hicho kiko tayari kumkaribisha. Naibu wa rais alisimama katika masoko ya Kambu, Kibwezi, Emali, Sultan Hamud na Salama.Ziara yake imewadia siku moja kabla ya kiongozi wa Wiper kuzuru kaunti ya Makueni hii leo.