Ruto Ampigia Debe Amina Mohammed Nchini Mali

Naibu wa Rais William Ruto amezindua awamu ya mwisho ya kampeini ya kumpigia debe waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Amina Mohammed A�kwa wadhifa wa mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika.Kampeini hiyo ilianza kwa ziara yake nchini Mali alikokutana na viongozi kadhaa miongoni mwao waziri mkuu wa Algeria Abdelmalek Sellal na rais Yoweri Museveni wa Uganda kando na kongamano la Ufaransa na mataifa ya Afrika kuhusu ushirikiano na amani lililoandaliwa mjini Bamako.