Ruto Adai Upinzani unatatiza Maandalizi Ya Uchaguzi

Naibu rais William Ruto sasa anadai kuwa upinzani una njama ya kushinikiza kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.Naibu rais alidai kuwa viongozi wa upinzani wanatatiza utaratibu wa kuhakikisha kwamba uchaguzi mkuu unaandaliwa vilivyo na tume huru ya uchaguzi, kupitia kesi mbali mbali mahakamani.Akiongea katika uga wa  Mumias Complex wakati wa ziara yake katika kaunti za Kakamega na  Bungoma,Ruto alisema upinzani umekwenda mahakamani kuzuia ukaguzi wa sajili ya wapiga kura na ununuzi wa makaratasi ya kura,hatua ambayo huenda ikachelewesha matayarisho ya uchaguzi mkuu.Naibu rais aliongeza kuwa  viongozi wa upinzani wanajaribu kuvuruga  mipango ya  tume ya uchaguzi  kwa vile hawako tayari kukabiliana na Jubilee kwenye uchaguzi mkuu.