Rudisha atarajiwa kung’aa nchini china kwenye riadha ya a�?Diamond Leaguea��

Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita mia nane David Rudisha, ni miongoni mwa wanariadha wa humu nchini wanaotarajiwa kunga��ara latika mkondo wa pili wa mashindano ya riadha ya a�?Diamond Leaguea�� utakaoandaliwa jijini Shanghai, Uchina Jumamosi hii. Rudisha alimaliza katika nafasi ya tano kwenye mkondo uo huo mwaka jana na atanuia kufanya vyema mwaka huu licha ya ukinzani mkali kutoka kwa wenzake Ferguson Cheruiyot na Alfred Kipketer. Faith Kipyegon, aliyevunja rekodi ya taifa ya mbio za mita 1500 na kunyakua nishani ya dhahabu ya Olimpiki jijini Rio, Brazil ni mwanariadha mwengine wa humu nchini anayeratarajiwa kufanya vyema nchini Uchina. Katika mashindano hayo, Kipyegon atalazimika kupambana dhidi ya Dawit Seyaum na Besu Sado wa Ethiopia. Wakenya wengine watakaoshiriki katika mkondo huo wa Shanghai ni Hellen Obiri na Hyvin Kiyeng.