Kamishna Roselyn Akombe ajiuzulu

Kamishna Roselyn Akombe wa tume huru A�ya uchaguzi na mipaka IEBC amejiuzulu,siku saba kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais.Kwenye taarifa A�Akombe alisema kwamba amelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na mibano na mivutano kutoka pande tofauti za kisiasa,ambayo haiwezi kuruhusu kufanywa kwa uchaguzi huru na wa haki.Aidha alisema rufaa nyingi zenye miegemeo kinzani A�kuhusu uchaguzi huo zimewasilishwa mahakamani. Akombe ambaye alikuwa amesafiri kwenda Dubai kusimamia uchapishaji wa karatasi za kupigia kura ya uchaguzi wa A�urais wa wiki ijayo,sasa ameelekea mjini New York akihofia usalama wa maisha yake.