Rodriguez asajiliwa kwenye kilabu cha Bayern Munich.

Kilabu cha Bayern Munich A�kinachoshiriki katika ligi kuu ya soka nchini Ujerumani kimemsajili mshambulizi wa Real Madrid, James Rodriguez A�kwa mkataba wa A�miaka miwili. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye alitia saini mkataba wa miaka sita kilabuni Real Madrid baada ya kusajiliwa kutoka Monaco kwa kima cha Pauni milioni 71 million mwezi Julai mwaka 2014, alicheza jumla ya mechi 22 za ligui kuu ya Uhispania A�msimu uliopita. Nahodha huyo wa Kolombia, hakujumuishwa kwenye kikosi cha Zinedine Zidane kilichoishinda Juventus kwenye fainali ya ligi ya kilabu bingwa barani Ulaya. A�A�Mchezaji huyo alikuwa amehusishwa kujiunga na vilabu vya Chelsea na Manchester United.