Rift valley Railways Yamteua Mkurugenzi Mkuu Mpya

Kampuni ya Rift Valley Railways imemteua Isaiah Otieno Okoth kuwa mkurugenzi wake mkuu mpya. Okoth anachukua mahali pa Carlos De Andrade aliyehudumu kwa kipindi cha miaka mitatu. Akitangaza hayo, mwenyekiti wa kampuni hiyo, Titus Naikuni amesema ujuzi wa Okoth katika masuala ya usimamizi utasaidia kampuni hiyo kufaulu katika shughuli zake. Uteuzi wa Okoth umewadia wakati ambapo kampuni hiyo imeingi kwenye hatua muhimu ya kujiimarisha baada ya miaka mitano ya uwekezaji ambapo imeweza kukunua injini kadhaa na mabehewa, mbali na kurekebisha reli na vile vile kuanzisha mipango ya kisasa wa usimamizi wa uchukuzi wa reli