Richard Onyonka achaguliwa tena

Richard Onyonka amechaguliwa tena kuwa mbunge wa A�Kitutu Chache kusini. Mwaniaji huyo wa chama cha A�Ford Kenya alishinda uchaguzi huo mdogo wa siku ya jumanne kwa kuzoa kura 10,122 ambayo ni asilimia 45.86 ya kura zilizopigwa. Onyoka atahudumia eneo bunge hilo kama mbunge kwa muhula wa tatu mfululizo. Afisa aliyesimamia uchaguzi katika eneo bunge hilo Hilda Imbo alimtangaza kuwa mshindi saa kumi usiku wa leo. Antony Kibagendi wa chama cha A�Jubilee alikuwa wa pili kwa kupata kura 5,074 huku A�Omwando Samwel Kenani akiibuka wa tatu kwa kura 4,324. A�Uchaguzi wa eneo hilo la Kitutu Chache kusini uliahirishwa mwezi Agosti kufuatia kifo cha mwaniaji wa chama cha Leonard Mwamb majuma mawili kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi huo. Onyoka mwenye umri wa miaka 55, alishinda kiti hicho mwaka wa 2007 kwa tiketi ya chama cha PDP. A�Mwaka wa A�2013, alishinda kiti hicho kwa tiketi ya chama cha ODM kwa kuzoa kura 17,274 dhidi ya kura 8,203 za mpinzani wake wa karibu wakati huo Don Bosco Gichana.