Rebecca Cherotich

Rebecca Cherotich ni mtangazaji stadi ambaye hukuletea kipindi cha 'Club Taifa' kila siku ya Ijumaa hadi Jumapili kuanzia saa mbili  hadi saa sita usiku.

Rebeccah ana shahada ya utangazaji kutoka Chuo Kikuu cha Kenya Methodist (KeMU)  na stashahada ya utangazaji kutoka  'East African School of Media Studies.'

Alipojiunga na shirika la utangazaji nchini KBC, Rebeccah alileta tajriba ya kupigiwa mfano ambayo imechangia pakubwa katika ufanisi wa kipindi cha 'Club Taifa'.

Licha ya kuwa binti mchangamfu, Rebecca ana uhusiano mwema sio tu na wafanyikaziwenza bali pia wasikilizaji kwa jumla wa Redio Taifa, anapenda kutazama sinema, michezo ya kuigiza, mwogeleaji hodari na msomi wa vitabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *