Rawal Amtaka Jaji Milton Kujiondoa Kusikiza Kesi Yake

Jaji Kalpana Rawal wa mahakama ya juu sasa anamtaka jaji Milton Makandia wa mahakama ya rufani kujiondoa kusikiza kesi yake kuhusiana na umri wa kustaafu kwa majaji. Mahakama ya rufani imemwagiza awasilishe ombi lake kufikia leo jioni. Majaji saba wa mahakama ya rufani wakiongozwa na GBM Kariuki walimwagiza Justice Rawal kuwasilisha ombi lake kutafuta kuondolewa kwa Justice Milton Makandia, kusikiza na kuamua kesi hiyo.