Ratiba ya Uhuru kuwa na shughuli nyingi mwezi huu

Rais Uhuru Kenyatta atakuwa na shughuli nyingi mwezi huu wa Mei, huku A�ratiba yake ikijumuisha majukumu ya hapa nchini na pia ya kigeni, mbali na maandalizi ya kampeini zake A�kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Augosti. Ratiba hiyo ya A�Rais Kenyatta, inaanza leo ambapo amepangiwa kuhudhuria kongamano la 26 la baraza kuu la shirika la umoja wa mataifa kuhusu mpango wa makaazi ya binadamu-(UN-Habitat). Kongamano hilo linatarajiwa kuweka msingi wa kisiasa, na pia mikakati ya utekelezaji wa ajenda mpya kuhusu makaazi ya sehemu za mijini. Hatibu wa Ikulu, Manoah Esipisu, alisema Rais Kenyatta atakuwa pia mwenyeji wa Rais Patrice Talon wa Benin mnamo wiki hii. Kisha baadaye, Rais Kenyatta atasafiri hadi London, Uingereza, kuhudhuria kongamano la tatu la London juu ya Somalia mnamo tarehe 11 mwezi Mei. Kongamano hilo A�linafuatia makongamano mengine mawili ambapo jamii ya kimataifa ilikubali kuelekeza juhudi mpya katika taratibu za kuleta uthabiti nchini Somalia. Baadaye, Rais Kenyatta ataelekea China, kuhudhuria kongamano kuhusu miundo msingi mnamo tarehe 15 mwezi Mei.