Rais Kenyatta amezindua tena huduma za feri za mtongwe

Rais Kenyatta amezindua huduma za feri za Mtongwe zilizosimamishwa miaka mitano iliyopita. Kurejelewa kwa huduma hizo ni afueni kwa wakazi wa Mtongwe kwani kutapunguza msongamano kwenye mapito makuu ya Likoni. Huduma za feri huko A�Mtongwe zilisimamishwa mwaka 2011 baada ya serikali kuondoa feri mbili zilizochakaa. Muundo msingi ulioharibika pia ulikuwa mojawapo wa sababu zilizoifanya serikali kuondoa huduma hizo za feri. Mnamo mwaka 1994, kwenye mojawapo wa jail mbaya zaidi za baharini humu nchini zaidi ya watu 270 walifariki kufuatia mkasa wa feri huko Mtongwe. Kuondolewa kwa feri hizo kulisababisha msongamano kwenye kivuko cha Likoni huku wakazi wa Mtongwe wakilalamika kwamba tangu kuondolewa kwa huduma hizo thamani ya nyumba zao imeshuka. Rais Kenyatta anafanya ziara ya eneo la pwani tangu siku ya Jumamosi ambapo amezindua na kukagua miradi kadhaa ya maendeleo.