Rais wa Zimbabwe asema Mugabe atapewa haki yake

Aliyekuwa rais wa Zimbabwe kwa muda mrefuA�Robert Mugabe hatahangaishwa na atapewa malipo yafaayo ya kustaafu kwa mujibu wa mrithi wakeA�Emmerson Mnangagwa. Hata hivyo Mnangagwa aliwaambia wanahabari kuwa hakuna yeyote ambaye amepewa kinga ya kushtakiwa. Raia wengi wa Zimbabwe wanatumai kuwa Mugabe na familia yake watashinikizwa kuwajibikia maisha ya kifahari waliokuwa wakiishi.

Mugabe aliondolewa mamlakani mwezi November baada ya kuwa uongozini kwa miakaA�37. Mnangagwa, ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Mugabe, walitofautiana akafutwa kazi na kutorokea nchini Afrika kusini kabla ya kurejea nchini humo na kutangazwa kuwa rais miezi miwili iliyopita. Ameahidi kupambana na ufisadi hasa miongoni mwa viongozi nchini humo.