Rais wa somalia aahidi kuiangamiza Al-shaabab

Rais wa Somalia Mohamed Abdulahi “Farmajo” ameelezea matumaini kuwa kundi la kigaidi la Al Shabaab litatokomezwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo. Rais huyo alisema jukumu la kuangamiza kundi hilo laweza kufikiwa kwa msaada wa jamii ya mataifa na kwamba wanajeshi wa nchi hiyo wamepata mafunzo  kamili  na wana uwezo wa  kulitibua kundi hilo la kigaidi. Alisema jeshi la nchi hiyo na kikosi cha kulinda usalama cha muungano wa Afrika-AU yanajiandaa kikamilifu kukabiliana na  kundi hilo la Al Shabaab. Rais Mohamed amekuwa mamlakani kwa miezi mitatu tu, ambapo  magaidi wa Al Shabaab wamefurushwa kutoka baadhi ya maeneo ya nchi hiyo  tangu lilipoanzisha harakati zake mwongo mmoja ulioppita. Kundi hilo lilikuwa likimiliki  sehemu kubwa za nchi hiyo kabla ya kuimarishwa kwa  harakati  dhidi ya wadwai wake.