Rais wa Peru awasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa baraza la Congress

Rais wa Peru amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa baraza la Congress nchini humo baada ya kutokea kwa kanda za videos ambapo washirika wake kadhaa wanadaiwa kupigwa picha wakijaribu kutafuta uungwaji mkono wa mbunge mmoja katika kura ya kutaka kumng’oa kiongozi huyo. Pedro Pablo Kuczynski mwenye umri wa  miaka 79 alitoa tangazo hilo katika hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye runinga ya taifa hilo siku moja kabla ya kura ya kumwondoa mamlakani kuhusiana na madai ya ufisadi kupigwa. Haikubainika iwapo bunge la Congress litakubali kujiuzulu kwake.