Rais wa Naigeria Muhammadu Buhari ahutubia taifa baada ya matibabu ya miezi mitatu

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amehutubia taifa baada ya kuwa nje ya nchi hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu akitibiwa mjini London. Katika hotuba yake kupitia runinga ya taifa, Buhari aliwashukuru raia wa Nigeria akisema ni furaha yake kubwa kurejea nchini humo.A�Buhari alisema alikuwa akifwatilia kwa makini yaliokuwa yakijiri nchini Nigeria na hasa dukuduku kuhusu kugawanyika kwa taifa hilo. Buhari alirejea nchini humo siku ya jumamosi kukiwa na tetesi za kutafuta mrithi wake. Hata hivyo, serikali ya Nigeria haijabainisha ni maradhi yapi anaugua rais huyo wa umri wa miaka-74. Mapema mwaka huu, Buhari alikuwa mjini London kwa matibabu. Nigeria inakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo vita dhidi ya kundi la wanamgambo la Boko Haram na msukosuko wa kifedha.