Rais wa misri atangaza hali ya dharura baada ya shambulizi la kigaidi

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ametangaza kipindi cha miezi tatu cha hali ya dharura kutokana na mshambulizi ya kigaidi yaliotekelezwa siku ya jumapili dhidi ya makanisa mawili ya kikoptiki,yaliosababisha vifo vya watu 44.Sheria za hali ya dharura zitaipa serikali mamlaka ya kuwatia washukiwa nguvuni bilaA� hati ya kuwakamata na pia kupekua nyumbva zao.Al-Sisi alitoaA� hotuba kali kuhusu swala hilo, muda mfupi baada yaA� kufanya mashauriano nyumbani kwake na baraza la ulinzi la kitaifa,ambapo walizungumzia mkasa wa milipuko hiyo miwili ya mabomu katika miji midogo ya Tanta na Alexandria wakati wa sherehe za kikristo za Jumapili ya mitende. Alionya kuwa vita dhidi ya magaidi wa kundi la Islamic StateA� vitakuwa virefu na vyenye madhara.Alisema sheria hizo za hali ya hatari zitaanza kutumika kikamilifu kote nchini baada tya hatua muafaka za kisheria na kikatiba kuchukuliwa.Awali rais Al-Sisi alikuwa ameamuru vikosi vya majeshi ya Misri kupelekwa kote nchini kulinda asasi muhimu ,ikiwemo miundomsingi.Kundi la Islamic State lilikiri kutekeleza mashambulizi hayo kupitia washambulizi wa kujitoa muhanga kufa dhidi ya makanisa ya kikoptiki ya St.Georges katika miji ya Tanta,ambako watu 27 waliuliwa na Alexandria ambako watu 17 waliangamia.Maafisa wa polisi ni miongoni mwa wale waliouliwa kwenye mikasa hiyo.Shambulizi hilo limetokea wiki chache kabla ya ziara inayotarajiwa nchini humo ya Baba mtakatifu Francis kama ishara ya kuunga mkono wakristo wachache walio nchini humo ,ambao ni aslimiaA� kumi ya jumla ya watu nchini humo na ambao wamelalamika kwa muda mrefu kwamba wamekandamizwa na kutengwa kwa muda mrefu.