Rais wa India astumiwa kwa madai ya kuwakejeli wahamiaji WA Bangladesh

Rais wa chama tawala nchini India amesekana kuwakejeli wahamiaji wa Bangladesh na kuzua gadhabu kali kutoka kwa Bangladesh na makundi ya kutetea haki za binadamu.

Katika matamshi ambayo alirudia mara mbili katika muda wa siku tatu zilizopita, Amit Shah ambaye ni rais wa chama cha mrengo wa kulia cha  Bharatiya Janata -BJP,  alisema kuwa mamilioni ya wahamiaji hao wameingia nchini humo kama mchwa na wanapaswa kufurushwa mara moja.

Alisema chama chake kitawarejesha makwao wahamiaji wote haramu iwapo atashinda uchaguzi mwaka ujao. Alitoa ahadi sawa na hiyo kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2014.