Rais wa Gambia Kung’atuliwa Mamlakani.

Senegal imeyapeleka majeshi yake kwenye mpaka wake na nchiA�A� Gambia katika juhudi za kumshurutisha rais Yahya Jammeh kunga��atuka uongozini baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa urais waA� mwezi Disemba mwaka jana.Senegal inaongoza operesheni hiyo ambayo pia inaungwa mkono na Nigeria na mataifa mengine ya kanda hiyo.Rais Jammeh ametakiwa kuondoka mamlakani kufikia leo jioni na kumkabidhi mamlaka mshindi wa uchaguzi wa urais Adama Barrow,ambaye kwa sasa yuko nchini Senegal.Jammeh ameitawala Gambia tangu alipotwaa mamlaka kupitia mtutu wa bunduki mnamo mwaka wa 1994.

Siku ya leo ingekuwa ya mwisho ya Jammeh kuwa mamlakani lakini bunge la nchi hiyo lilimwongezeaA� kipindi cha utawala cha miezi mitatu.Katibu wa rais wa Nigeria Muhamadu Buhari alisema kuwa Barrow anajiandaa kutawazwa kesho kuwa rais mpya wa Gambia.Takriban raia 26,000 wa GambiaA� wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Senegal wiki hii wakihofia usalama wao.