Rais Uhuru Kuzuru Makueni Na Kitui

Rais Uhuru Kenyatta leo atazuru kaunti za Makueni na Kitui kuzindua na kukagua miradi ya Maendeleo. Miradi hiyo katika sekta ya barabara na afya ni sehemu ya miradi ya Maendeleo A�itakayogharimu shilingi bilioni 144 zilizowekezwa na serikali ya Jubilee katika eneo la mashariki. Rais A�Kenyatta atazindua huko Sultan Hamud kaunti ya Makueni mradi wa kuweka lami utakaogharimu shilingi biliobni 1.2 barabara kati ya Kasikeua��Wautua��Kyambeke na Kikoko na pia kuwahutubia wananchi. Baadaye atakwenda A�Mbooni kukagua ujenzi wa chuo cha mafunzo ya kimatibabu cha Mbooni kabla ya kukutana na viongozi na wakazi kujadili Maendeleo. Wakati wa alasiri Rais atakuwa huko Mutomo, kaunti ya Kitui kuzindua ukarabati wa barabara kati ya A�Kibwezia��Mutomo na Kitui. Atakamilisha siku ya kwanza ya ziara yake kwa kuzindua mradi wa kuweka lami barabara kati Kibwezi na Mutomo. Baadaye atahutubia mkutano wa hadhara katika shule ya upili ya wasichana ya A�St. Joseph Girls huko Kibwezi.