Rais Uhuru kenyetta Azuru Mradi wa Ujenzi wa Makazi ya Kampuni ya Karibu homes Riverview Huko Athi river

Rais Uhuru Kenyatta alizuru mradi wa ujenzi wa makazi wa kampuni ya Karibu Homes Riverview ambao unafadhiliwa na taasisi ya kifedha ya Shelter Afrique wa ujenziA� nyumba za gharama nafuu huko Athi River katika kaunti ya Machakos.

Rais aliongoza kamati ndogo ya baraza la mawaziri kuhusu nyumba akiwemo naibu rais William Ruto kwenye ziara ya kukadiriaA� mradi huo ili kujifahamisha na mradi huo wa nyumba za gharama nafuu kwa lengo la kujenga nyumba za gharama nafuu kwa matumizi ya serikali.

Nyumba hizo zenye vyumba viwili na vitatu vya malazi, zinajengwa na kampuni ya Karibu Homes Riverview ambayo hujenga nyumba za makazi na kibiashara kutokana na ufadhili wa taasisi ya kifedha ya Shelter Afrique.

Shelter Afrique ni taasisi ya kifedha ya kufadhili ujenzi wa nyumba barani Afrika ambayo inafadhili ujenzi wa nyumba hapa nchini na katika mataifa mengine 43 ya bara hili. Akiongea na baadhi ya wahudumu kwenye mradi huo, rais alisema serikali inachunguza mradi huo wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa Wakenya.