Rais Uhuru Kenyatta Awasili Brussels, Belgium Kwa Ziara Ya Siku Tatu

Rais Uhuru Kenyatta amewasili jijini Brussels, Ubelgiji kwa ziara ya siku tatu , ambapo atatoa hotuba muhimu kwenye siku ya maendeleo barani Ulaya na kufanya mikutano kadhaa ya pande mbili kuhusu biashara na usalama. Katika hotuba yake Rais Kenyatta anatarajiwa kuwaelezea viongozi wa Jumuiya ya Ulaya na viongozi wa nchi na serikali walioalikwa tajiriba iliyo nayo Kenya. Pia anatarajiwa kuelezea mtazamo wa Kenya kuhusu ushirikiano wa siku zijazo na ushirikiano wa kimaendeleo. Rais amepangiwa kufanya mikutano ya pande mbili na maafisa wa ngazi ya juu wa Jumuiya ya Ulaya akiwemo Rais wa Jumuiya hiyo ya EU Jean Claude Juncker na Rais wa Baraza la Ulaya Donal Tusk. Pia Rais Kenyatta anatarajiwa kufanya mikutano ya faragha na waziri Michel na Phillipe. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifaA�Ban Ki-Moon na rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim, pia wanahudhuria mkutano huo ambao maudhui yake ni a�?Kuendelea kwa hatua ya malengo ya maendeleo endelevua�?: Dubia yetu, hadhi yetu, Hatima yetua�?.