Rais Kenyatta ahimiza wanasiasa kuwahudumia wakenya

Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wanasiasa wazingatie kuwahudumia Wakenya badala ya kueneza siasa za kupotosha na sarakasi zisizo na maana. Kadhalika rais alisema wakati wa malumbano ya kisiasa umekwisha na viongozi sharti waanze kufanya kazi kwa bidii ili watimizeA�A�matakwa na matarajio ya wapiga kura. Rais alisema Wakenya waliwachagua viongozi wao wakati wa uchaguzi mkuu uliopita akiongeza kusema kwamba kwa sasa hawatarajii siasa za kupotosha na sarakasi zisizo na maana. Rais alisema haya katika kaunti ya Kajiado ambako alizindua kiwanda cha kutengeneza saruji cha dolla milioni 280 ambacho kimebuni nafasi 700 za ajira na nafasi hizo zinatarajiwa kuongezeka mara kumi katika muda wa miaka miwili ijayo. Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku na mwenzake wa Machakos, Alfred Mutua, walikariri matamshi ya rais kwamba Wakenya wapasa kuzingatia utenda kazi ambao utastawisha nchi hii kwani msimu wa kampeni umepita. Gavana Lenku aliahidi kuunga mkono ajenda nne kuu za rais akisema hiyo ndio njia ya kuafikia malengo ya maendeleo ya nchi hii.