Rais Uhuru Kenyatta awaambia wajumbe kutoka chama cha Jubilee kudumisha umoja

RaisA� Uhuru Kenyatta jana aliwaambia wajumbe kutoka chama cha Jubilee na vyama vyake tanzu kudumisha umoja na malengo yao ili kuhakikisha kuwa anapata ushindi mkubwa zaidi katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa kurudiwa tarehe 26 mwezi ujao wa Oktoba.A� Rais alitoa wito kwa wajumbe hao kujitahidi na kuhakikisha kuwa chama cha Jubilee kinafaulu ili kukiwezesha kuendeleza ajenda yake ya marekebisho kwa wakenya wote. Rais ambaye alikuwa ameandamana na naibu wake William Ruto katika mkutanoA� ulioandaliwa katikaA� ikulu ya Nairobi alisema kuwa chama cha Jubilee na vyama vyake washirika kinashindana na wapinzani wake katika mazingira ya kisiasa yaliyojawa uhasama wa kikabila. Hata hivyo alisema kuwa baada ya uchaguzi huo, chama chaA� Jubilee kitaidhinishwa tena kama chama kinachojali maslahi ya wakenya wote. Naibu wa rais alisema kuwa chama chaA� Jubilee kinashughulikia mikakati inayolenga kuongeza na kupata wingi wa kura.A� Alisema kuwa chama cha Jubilee kinataka kuhakikisha kuwa kinakuwa na waakilishi wa kuaminika na wakakamavu wa chama hicho ambao wanaelewa mchakato wa kupiga kura ili kujihakikishia ushindi. Wengine waliohudhuria mkutano huo ni magavana wa zamani John Mruttu ambaye alikuwa wa kaunti ya Taita Taveta, Peter Munya ambaye alikuwa wa kaunti ya Meru, Moses Akaranga ambaye alikuwa wa kaunti ya Vihiga, Hussein Dado wa Tana River na aliyekuwa mwenyekiti wa chama chaA� Wiper ambaye pia aliwania kiti cha ugavana katika kaunti ya Kitui David Musila.