Rais Uhuru Kenyatta Atarajiwa Kutoa Taarifa Maalum Kuhusiana Na Chama Cha Jubilee

Rais Uhuru Kenyatta leo asubuhi anatarajiwa kutoa taarifa maalum kuhusiana na chama cha Jubilee. Taarifa hiyo itatangazwa mubashara kutoka ikulu ya Nairobi,kwa mujibu waA� kitengo cha mawasiliano cha rais-(PSCU).Tangazo hilo linafwatia kubuniwa kwa chama cha Jubilee ambacho rais Uhuru atakitumia kuwa nia awamu ya pili ya uongozi.Haya yanajiri huku kukitokea mabadiliko ya kimirengo ya kisiasa hapa nchini.

Wakati uo huo rais Uhuru KenyattaA� katika ikulu ya Nairobi alikutana na Katshuyuki Kawai,mshauri mkuu wa waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na kujadili maswala kuhusiana na kongamano lijalo la TICAD VI.