Rais Uhuru Kenyatta Asisitiza Kuwa Naibu Rais William Ruto Angali Chaguo Lake La Kumrithi

Rais A�Uhuru Kenyatta amesema anamuunga mkono kikamilifu naibu rais William Ruto katika siasa za urithi. Kupitia mkurugenzi wa mawasiliano A�A�katika ikulu ya Nairobi A�Munyori Buku, rais amesisitiza kuwa William A�Ruto, angali chaguo lake la kumrithi baada ya kukamilika kwa hatamu yake ya pili mwaka 2022. Kwenye taarifa Munyori amesema mipango ya maendeleo ya serikali ya muungano inahitaji muda wa jumla ya miaka 20 kukamilishwa A�na muda huo unaweza tu kutimizwa na naibu rais aliye mamlakani. Kwenye taarifa hiyo rais amesema matamshi ya seneta maalum Paul Njoroge kuwa hakuna hakikisho kuwa A�Ruto atamrithi mwaka 2022 ni ya kiholela na hayawiani na maoni yake. Taarifa hiyo imejiri siku moja baada ya seneta maalum Paul Njoroge kusema A�Ruto hafai kuwashurutisha wapiga kura wa eneo la kati kuhusiana na azma yake ya kuwania urais mwaka A�2022.