Rais Uhuru Azitaka Nchi Kiafrika Kushirikiana Ili Kuafikia Ajenda Ya Maendeleo

Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa nchi za kiafrika zinafaa kushirikiana ili kuafikia ajenda yao ya maendeleo. Akiongea katika kikao cha 14 cha kongamano la umoja wa mataifa kuhusu biashara na maendeleo kinachofanyika jijini Nairobi kilichoingia siku yake ya pili jana, rais Kenyatta alisema mashirika kama yale ya umoja wa mataifa ni sharti yashirikiane na serikali za kitaifa na makundi ya kijamii katika nchi husika ili kuoata suluhu kwa changamoto zinazokabili bara hili.
Rais alitoa wito wa kufanyiwa mabadiliko kwa umoja wa mataifa ili kuimarisha utenda kazi wake. Alisema umoja huo utafanikiwa kutatua mizozo endapo utashirikiana na serikali za taifa na viongozi katika kutatua mizozo ibuka.