Rais Uhuru Ataka Wanawake Na Wanaoishi Na Ulemavu Wapewe Umuhimu Wa Kwanza

Rais Uhuru Kenyatta jana aliongoza mkutano wa sita wa baraza la mawaziri ambapo aliziagiza wizara za serikali kuwalipa wawasilishaji bidhaa,umuhimu wa kwanza ukipewa wanawake,vijana na watu wanaoishi na ulemavu .Wakati wa mkutano huo,baraza la mawaziri liliidhinisha ushirikiano kati ya serikali na kampuni ya kutengeneza sarafu ya De La Rue, ambapo serikali itanununua asilimia 40 ya hisa kwenye kampuni hiyo.Baraza la mawaziri pia liliiagiza wizara ya usalama wa taifa na vitengo vya usalama kuwakamata na kuwashtaki wale wanaovamia mashamba ya ufugaji ya binafsi katika kaunti za Laikipia,Kilifi na kwingineko nchini. Na katika kuendeleza ushirikiano wa Afrika Mashariki ofisi zote za serikali na taasisi za umma,zikiwemo shule sasa zithitajika kupeperusha bendera ya jumuiya ya Afrika mashariki,huku wimbo wa jumuiya hiyo ukiimbwa sambamba na ule taifa shuleni na hata wakati wa hafla za kitaifa.