Rais Uhuru Ashutumu Upinzani Kwa Kuvamia Afisi Za IEBC

Rais A�Uhuru Kenyatta kwa siku ya pili mfululizo ameushtumu upinzani kwa kutumia mbinu zisizofaa kuvamia afisi za tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini – IEBC huku akisisitiza kuwa katiba inaratibu taratibu ambazo zinastahili kufuatwa katika kuwaondoa makamishna walioteuliwa kikatiba. Rais A�Kenyatta ambaye anafanya ziara katika kaunti ya Kisii aliushtumu upinzani huku akisisitiza kuwa Wakenya wana usemi mkubwa kuliko dhana yoyote ya kisiasa. Kaunti ya Kisii na eneo la magharibi ya nchi kwa ujumla linaaminika kuwa ngome ya upinzani. Rais Kenyatta ambaye alikuwa ameandamana na naibu wa rais William Ruto na maafisa kadhaa wakuu wa serikali, alisema kuwa wapiga kura ndio watakaoamua mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2017 hata kama tume mpya ya IEBC itateuliwa. Rais Kenyatta alitoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kuzingatia siasa za kuleta maendeleo na kukoma kuwasikiza viongozi ambao lengo lao ni kuwagawanya Wakenya.