Rais Uhuru Asema Ufisadi ni Kikwazo Kwa Maendeleo

RaisA� Uhuru Kenyatta amesema kuwaA� ufisadi hapa nchini ndio kikwazo kikubwa zaidi kwa maendeleo ya kitaifa.Alisema kuwa tayari kuna zaidi ya kesi 360 za ufisadi zinazoshughulikiwa na tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi. Rais alisema kuwa serikali yake imejitoleaA� kuwafungulia mashtaka wale wote waliohusika katika ufisadi .Vita dhidi ya ufisadi pia viliimarishwa kwa kutengwa kwa shilingi bilioni 1.9 za kuharakisha uchunguzi na kushtakiwa kwa watakaopatikana na hatia. Alitoa changamoto kwa idara ya mahakama kutekeleza jukumu lake na kuwashtaki waliohusika bila kuchelewa. Rais alisema kuwa tayari serikali yake imetambua ziliko mali za shilingi bilioni 1.6 na shilingi milioni 400 zaidi za hazina ya vijana .

Ugaidi pia ni changamoto nyingine ambayo imeathiri uchumi wa nchi hii huku nafasi nyingi za ajira zikipotezwa katika sekta ya utalii. Rais hata hivyo alisema kuwa serikali yake imeweka mikakati ya kufufua sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kutenga shilingi bilioni 1.2 za kufufua sekta ya utalii .A� Alisema pia kuondolewa kwa ada za visa kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 16 kuanzia mwezi Februari kutasaidia pakubwa katika kuimarisha sekta hiyo.