Rais Uhuru Amkabidhi Waziri Wa UChimbaji Madini, Dan Kazungu Sheria Ya Mwaka Huu Ya Uchimbaji

Rais Uhuru Kenyatta jana alimkabidhi waziri wa uchimbaji madini Dan Kazungu sheria ya mwaka huu ya uchimbaji kwa utekelezaji. Sheria hiyo aliyoitia saini mwezi uliopita inatoa mwongozo kamili kuhusu shughuli za uchimbaji madini nchini. Rais aliikabidhi sheria hiyo kwa waziri katika ikulu ya Nairobi, kabla ya kusafiri kwenda Angola kuhudhuria kongamano la sita la kimataifa kuhusu eneo la maziwa makuu hii leo.

Akipokea nakala ya sheria hiyo mpya waziri wa utalii alielezea imani yake kuwa sheria hiyo italainisha sekta hiyo nchini, kuiwezesha kukua na kuhakikisha uhifadhi mazingira. Kazungu alisema kuwa sheria hiyo inatoa hakikisho litakalowezesha upanuzi wa haraka na maendeleo endelevu katika sekta hiyo. Alisema sheria hiyo ni mojawapo wa zile zitakazoleta maendeleo makubwa katika sekta ya uchimbaji madini barani Afrika.