Uhuru amesema vijana wana jukumu la kujisajili ili washiriki kwenye uchaguzi mkuu

Rais Uhuru Kenyatta amesema vijana hapa nchini wana jukumu la kujisajili kuwa wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao. Rais alisema hali ya sasa na baadaye ya nchi hii inawategemea vijana na wapasa kuimarisha ushiriki wao katika masuala ya taifa hili. Rais Kenyatta alisema vijana ni thuluthi mbili ya raia wa nchi hii na hiyo inamaanisha kwamba wana uwezo wa kuwachagua viongozi wanaozingatia maslahi yao. Rais Kenyatta alisema haya alipokutana na wasanii mashuhuri akiwemo mwimbaji wimbo za injilitia Roy Smith Mwatia ambaye pia anajulikana kama a�?Rufftonea�? na mtangazaji mashuhuri wa Redio Daniel Githinji Mwangi almaarufu a�?Mbusia�? katika ikulu ya Nairobi. Rais alisema vijana wapasa kujisajili kwa wingi ili kuwapigia kura viongozi ambao hawatazingatia ukabila na ufisadi na ambao watabuni fursa za biashara na ajira. Leo rais kwanza atafungua kongamano la kibiashara kati ya Kenya na Ujerumani kabla ya kuzuru sehemu mbali mbali za kaunti ya Nairobi. Kesho rais atazuru kaunti ya Nyandarua na siku ya Jumamosi atazuru kaunti ya Nakuru.