Rais Uhuru Ahimiza Kampuni Za India Kuwekeza Humu Nchini

Rais Uhuru Kenyatta amehimiza kampuni zaidi za India kuwekeza hapa nchini ili kuondoa nakisi ya kibiashara kati ya Kenya na India ambapo kwa wakati huu India ndiyo inanufaika zaidi. Rais aliitaka India kufungua masoko yake kwa bidhaa za Kenya na kusaidia katika mikakati ya kuongeza thamani kwenye bidhaa hizo. Rais Kenyatta alisema kampuni za India zinazoendesha shughuli zao hapa nchini zinafurahia mazingira bora na salama ya kibiashara na uwekezaji. Akihutubu jana jioni kwenye kikao cha pamoja cha ujumbe wa wafanyibiashara kutoka Kenya na India jijini Nairobi ambacho kilihudhuriwa na waziri mkuu wa India,A�Narendra Modi, rais Kenyatta alisema Kenya imebuni mazingira bora ya kuvutia biashara na uwekezaji kutokana na soko lake pana na hali yake ya kijiografia katika kanda hii na kimataifa

Naye waziri mkuu, Narendra Modi alisema serikali yake itasaidia Kenya kuwa kitovu cha huduma za matibabu katika eneo hili. AlisemaA�Kenya ana India zitashirikiana katika miradi ya kuzalisha kawi kutokana na jua ili kufanikisha usambazaji umeme vijijini.

Modi na Kenyatta waliahidi kuwasaidia wafanyabiashara kutoka nchi hizo mbili kufikia upeo wao wa kiuchumi kupitia ushirikiano. Biashara kati ya Kenya na India ilifikia shilingi trilioni-9.4 mwaka-2013 kutoka shilingi trilioni-5.1 mwaka-2009.