Rais Trump afutilia mbali mpango wa kuwalinda wahamiaji wasiokuwa na stakabadhi zozote

Rais, Donald Trump wa Marekani ameamua kufutilia mbali mpango wa kuwalinda wahamiaji chipukizi wasiokuwa na stakabadhi zozote. Trump amelipa bunge la Congress muda wa miezi sita kubadilisha mpango huo wa kuwalinda wahamiaji chipukizi. Hata hivyo baadhi ya wadadisi wamsema rais Trump anaweza kubadili uamuzi wake. Mpango huo wa Daca unaruhusu maelfu ya vijana wanaoingia nchini Marekani kusoma na kufanya kazi hata bila stakabadhi halisi.