Rais Omar al-Bashir amtimua mkuu wa idara ya ujasusi

Rais Omar al-Bashir wa Sudan amemtimua mkuu wa idara ya ujasusi nchini humo, Mohammed Atta huku msako ukiendelea dhidi ya waandamanaji wanaolalamika kuhusu bei ya juu ya vyakula. Bashir amemteua Salah Abdallah Mohammed Salih kuwa mkuu mpya wa idara ya ujasusi ingawa hakutoa maelezo yoyote. Salih alikuwa akiongeza idara hiyo kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Atta mwezi agosti mwaka-2009. Waandamanaji wamekuwa wakilalamika kwa wiki kadhaa baada ya bei ya mkate kupanda kutokana na hatua ya kuruhusu sekta ya binafsi kuagiza ngano na hivyo kuchochea kupanda kwa bei ya unga wa ngano.