Rais Obama Atoa Hotuba Yake Ya Mwisho

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa hotuba yake ya mwisho kwa taifa jimbo la Chicago,ambapo ameakisi muda wa huduma yake kwa taifa katika wadhifa huo na kusema kuwa taifa hilo limezidi kuwa A�kuu hasa katika kipindi chake cha utawala cha miaka 8.Aliwataka wamarekani wa kila tabaka kustahiana na kusikiza maoni ya wenzao na kusema jambo hilo ni muhimu.Rais Obama ,ambaye alikuwa wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kutawala taifa hilo, na ambaye sasa ametimiza umri wa miaka 55 alichaguliwa rais mnamo mwaka wa 2008 kwa ahadi ya A�kuleta tumaini na mabadiliko.Mrithi wake rais mteule Donald Trump ataapishwa kuwa rais mpya tarehe 20 mwezi huu na ameapa kubadili sera muhimu za A�mtangulizi wake.Obama alisema sherehe ya amani ya kukabidhi mamlaka imekuwa nembo ya katika demokrasia ya A�Marekani.