Rais Nicolas Maduro ataja vikwazo vya Marekani kuwa visivyo na msingi

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametaja vikwazo vya Marekani dhidi ya utawala wake kuwa visivyo na msingi huku shinikizo zikiongezeka dhidi yake kuhusiana na mpango wake tata wa kuchagua jopo jipya kuandika upya katiba ya taifa hilo. Hatua hiyo ya marekani iliwadia huku upinzani nchiniA� Venezuela ukianza siku mbili za mgomo wa kitaifa unaolenga kumwondoa mamlakani rais huyo kupitia kwa uchaguzi wa mapema. Upinzani umepanga maandamano mengine makubwa katika mji mkuu wa taifa hilo siku ya ijumaa.