Rais mustaafu wa Africa Kusini Mbeki, ashtumu chama tawala kwa kuwa cha Waafrica pekee

Aliyekuwa Rais wa Afrika kusini Thabo Mbeki, amekishtumu chama tawala cha (ANC), na kusema kimegeuzwa kuwa cha Waafrika pekee. Mbeki alitamka hayo huku akikosoa umuzi wa chama hicho kunyakua mashamba yanayomilikwia na wazungu bila fidia yoyote.

Alionya kwamba chama cha (ANC) kinawalenga watu weupe na kimesahau ahadi za kuepukana na ubaguzi wa rangi. Chama hicho kinaendeleza sera ya kuleta usawa katika umiliki wa ardhi.

Karibu nusu karne baada ya kutamatishwa kwa mfumo wa utawala wa ubaguzi wa rangi, watu weupe ambao ni asilimia 9 ya idadi ya raia wa taifa hilo wanamiliki  asilimia 72 ya mashamba kulingana na takwimu za serikali.