Donald Trump Aahidi Kuunganisha Amerika

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameahidi kuliunganisha taifa la Marekani, Trump aliyasema haya kwenye hotuba kwa wafuasi A�wake mjini Washington DC, mkesha wa kuamkia leo ambapo ataapishwa kuwa rais A�wa Marekani.Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo iliodumu saa mbili ni msanii muigizaji Jon Voight na mwimbaji Sam Moore.Shughuli ya kumwapisha Trump kuwa rais mpya wa Marekani A�itaongozwa leo na jaji mkuu wa mahakama ya juu nchini humo John Roberts na kuonyeshwa moja kwa moja duniani kupitia runinga.Marais watatu wa mwisho wa taifa hilo wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo,akiwemo aliyekuwa mwaniaji wa urais wa chama cha Democratic Bi.Hillary Clinton.