Rais Mtaafu Daniel Moi Apinga Pendekezo La Kufutilia Mfumo Wa Elimu Wa 8-4-4

Rais mstaafuA�Daniel arap Moi amepinga pendekezxo la kufutilia mbali mfumo wa elimu wa nane-nne-nne. Akiongea jana kwenye ibada ya kutoa shukurani katika shule yaA�Sunshine jijini Nairobi, Moi alitetea mfumo wa elimu wa nane-nne-nne ulianzishwa baada ya utafiti wa kina na ulinuiwa kuwawezesha wakenya kupata elimu bora kimataifa. Moi alisema wengi wa wanafunzi ambao wamepitia mfumo huo wamejiunga na vyuo vikuu bora zaidi duniani ambapo wamefuzu na kupata ajira katika ngazi za kimataifa. Alisema mfumo huo ni mojayapo ya mafanikio ambayo nchi hii imepata.A�Moi alionya dhidi ya hatua ya kuharakisha kubunia kwaA� mfumo mwingine wa elimu bila kuzingatia uwezo wa kiuchumi wa nchi hii wa kukimu mahitaji ya kifedha ya shughuli hiyo.