Rais Mstaafu Moi Aibua Wasiwasi Dhidi Ya Ufisadi Nchini Kenya

Rais mstaafu,A�Daniel Arap Moi ametoa wito kwa wakenya wote kuisadia serikali kukabiliana na ufisadi ambao umekithiri hapa nchini. Akiongea wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa la AIC mjini Kapsabet, Moi alisikitishwa na jinamizi la ufisadi hapa nchini na kuwataka viongozi kuzingatia zaidi swala la maendeleo hapa nchini. Moi alisema ufisadi umekuwa kizingiti kikuu kwa juhudi za kuafikia upeo wa maendeleo katika taifa hili. MoiA�hakugusia swala la siasa hususan uchaguzi mdogo unaoendelea katika kaunti ya Kericho ambako chama chaA�JAP kinakabiliwa na upinzani kutoka kwa chama cha KANU. Aliwahimiza wakenya kutekeleza wajibu wao katika kukabiliana na uovu huo akisisitiza haja ya viongozi hapa nchini kuonesha uwajibikaji.