Rais Kwenyatta awakosoa wapinzani wake akiwa katika kampeini zake Kisii

Rais Uhuru Kenyatta jana alisema baadhi ya madai ya upinzani katika siku za hivi punde kuhusu hali ya uchaguzi ni ishara kwamba wamehisi kushindwa. Rais alisema kwamba upinzani jinsi ulivyo kwa sasa unaonyesha hauko tayari kuliongoza taifa hili. Rais aliukosoa upinzani kwa kutokuwa na maono na mipango kamili ya kuendeleza ufanisi ambao taifa hili limeshuhudia.A�A�Aidha alimtahadharisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga dhidi ya kumsuta waziri dakta Fred Matianga��i na kuwagawanya wakenya kwa misingi ya ukabila.A�Naibu wa rais William Ruto ambaye pia alihudhuria mkutano huo wa Kisii alitoa wito kwa wakenya wamuunge mkono rais Kenyatta ili kuhakikisha kiwango cha ukuaji wa uchumi wa nchi hii. Alisema Kenya imepanda kutoka nafasi ya 137 hadi 92 katika urahisi wa kufanya biashara duniani kufuatia mikakati ya kimaendeleo na uwekezaji iliyowekwa na serikali ya Jubilee katika sekta mahsusi kama vile miundo msingi na usalama.A�