Rais Kenyatta na William Ruto wapeleka kampeini zao Kericho na Nakuru

RaisA� Uhuru Kenyatta pamoja na naibu wake William Ruto leo watahutubia mkutano wa kampeni katika uwanja wa kihistoria wa Kapkatet, kaunti ya Kericho. Gavana wa Kericho, Paul Chepkwony amewahimiza wakazi wa kaunti za Kericho na Bomet kujitokeza kwa wingi kuwakaribisha vinara hao wa chama cha Jubilee. Rais Uhuru Kenyatta pia atahutubia wananchi katika miji ya Nakuru na Naivasha. Rais atakamilisha awamu ya kwanza ya kampeni zake hapo kesho jijii Nairobi. Wakati huo huo, muungano waA� NASA ukiongozwa na Raila Odinga utaandaa mikutano yake ya kampeni katika kaunti ya Machakos baada ya kupeleka kampeini zake katika kaunti za Kisii na Nyamira.