Rais Kenyatta kuzuru Marsabit na Samburu

Rais Uhuru KenyattaA�leo atazuru kaunti za Marsabit na Samburu kwenye msururu wa kampeni zake za kuwarai wapigaji kura kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi agosti. Rais Kenyatta anatafuta uungwaji mkono wa wakazi wa kaunti hizo ambao walipigia kura upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013. Uhuru ameimarisha kampeni zakeA�zikisalia siku chache kabla ya uchaguzi mkuu.A�Katika kipindi cha siku zilizosalia,A�A�rais Kenyatta na naibu wake William Ruto wanatarajiwa kuzuru kaunti za Bungoma, Kakamega, Elgeyo Marakwet, Baringo, Embu, Kirinyaga, Kiambu, Kajiado, Nakuru, Nyandarua, Laikipia,A� Bomet, Kericho, Meru, Tharaka Nithi, Kitui, Kilifi, Mombasa, Kisii, Nyamira, Nandi, Garissa, Migori, Uasin Gishu na Nairobi. Kampeni ya mwisho ya rais itaandaliwa jijini Nairobi tarehe-6 mwezi agosti, saa 48 tu kabla ya siku ya uchaguzi mkuu.