Rais Kenyatta kuzuru China kwa mashauriano kuhusu maendeleo

 Rais Uhuru Kenyatta mwishoni mwa wiki anatarajiwa kuondoka hapa nchini kuelekea mjini Beijing ambako atahudhuria mkutano wa kujadilia ushirikiano kati ya China na mataifa ya bara la Afrika.

Rais Kenyatta anatarajiwa kushauriana na maafisa wakuu wa serikali ya China wakati wa kikao hicho kitakachoandaliwa jumatatu wiki ijayo.La kwanza kwenye ajenda ya Kenya litakuwa kutiwa saini kwa muafaka wa mkopo wa shilingi billion 380 za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa kati ya Naivasha na Kisumu.

Ujenzi wa reli hiyo kutoka Mombasa hadi Nairobi uligharimu shilling billion 327 na wa sehemu ya kuelekea Naivasha kugharimu shilling billioni 150.Wakati wa mahojiano na shirika moja la habari la China, Rais Kenyatta alisema Kenya itaendelea kushirikiana na China katika kuimarisha miundo msingi ya nchi hii na vile vile kushirikiana na sekta ya kibinafsi katika ufadhili wa miradi ya maendeleo.Rais Kenyatta alisema miradi ya ustawishaji miundo msingi hii inayofadhiliwa na serikali ya China inasaidia kuiamrisha uchumi wa Afrika.