Rais Kenyatta Azindua Msaada Wa Masomo Ya Uhandisi Wa Reli Kwa Wanafunzi 25

Rais Uhuru Kenyatta leo alizindua mpango wa msaada wa masomo utakaowapa mafunzo wahandisi wapya wa Reli nchini China ambao watasimamia reli ya kisasa iliyo chini ya ujenzi hapa nchini.Rais alikuwa mwenyeji wa wanafunzi 25 watakaojiunga na masomo ya uhandisi katika chuo kikuu cha Jiaotong mjini Beijing kupitia mpango wa msaada wa karo utakaofadhiliwa na kampuni ya ujenzi wa miundo msingi ya uchukuzi ya China.Sherehe hiyo iliandaliwa katika ikulu ya Nairobi ambapo rais aliwahimiza wanafunzi hao kufanya bidii masomoni ili kuinufaisha nchi hii siku zijazo.Wanafunzi hao 25 ni kundi la kwanza la wanafunzi 60 ambao wamechaguliwa kwa mafunzo ya shahada ya degree ya uhandisi wa reli.Rais Kenyatta alisema serikali imejitolea kufufua na kuimarisha uchukuzi wa reli nchini na akaishukuru serikali ya China kwa kushirikiana na Kenya.