Rais Kenyatta Atuma Rabirabi Zake Kutokana Na Kifo Cha Boutrous

Rais Uhuru Kenyatta amemuenzi aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Boutrous Boutrous-Ghali aliyeaga dunia jana mjini Cairo. Boutros-Ghali, ambaye amekuwa balozi wa Misri, alikuwa katibu mkuu wa kwanza wa umoja wa mataifa kutoka bara Afrika. Rais Kenyatta alimsifuA� Boutros-Ghali kwa mapendekezo ya marekebisho ya umoja wa mataifa aliyopendekeza alipokuwa mamlakani. Kiongozi huyo atakumbukwa kwa mapendekezo aliyoyatoa katika ripoti zake mbili kuu kwa baraza kuu la umoja huo moja; ile ya ajenda ya amani na nyingine ya maendeleo.A� Kulingana na rais, Boutros Ghali alikuwa mbunifu wa kimawazo, na mapendekezo yake yameleta mabadiliko katika nyanja kama vile uhifadhi amani.