Rais Kenyatta Atia Saini Mswada Wa Ugavi Wa Raslimali Kuwa Sheria

Rais Uhuru Kenyatta leo asubuhi alitia saini kuwa sheria mswada wa ugavi wa raslimali kwa serikali za kaunty wa mwaka huu.Sheria hiyo itahakikisha ugavi sawa wa raslimali za kitaifa kati ya serikali za kaunty zote.Pia inaweka kiwango cha pesa ambazo serikali za kaunty zinastahili kutumia kwa mishahara ya wafanyikazi wake na shughuli nyingine za serikali za kaunty hizo.Sheria hiyo inaorodhesha ruzuku zote ambazo serikali za kaunty zinapokea kutoka kwa serikali ya kitaifa.Pia inapendekeza hazina kuu iwe ikichapisha ripoti ya kila mwezi ya migao yote ya pesa inazotoa kwa serikali za kaunty.Kila hazina ya kaunty itahitajika kuonyesha pesa zote inazopokea kutoka kwa serikali kuu kwenye vitabu vyake vya hesabu za pesa.Mswada huo uliwasilishwa na spika wa bunge la senate Ekwe Ethuro kwa kiongozi wa taifa ili autie saini.