Rais Kenyatta Atia Saini Mswada Wa Ugavi Wa Mapato 2016

Rais A�Uhuru Kenyatta ametia saini kuwa sheria mswada wa ugavi wa mapato wa A�mwaka 2016 pamoja na mswada wa A�makadirio ya ziada . sheria ya ugavi wa mapato inawezesha usambazaji sawia wa A�mapato yanayopatikana kitaifa kati ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti A�katika kipindi cha bajeti cha mwaka A�2016/17 . mapato yanayopaswa kugawanywa katika mwaka 2016/2017 ni shilingi bilioni 1,380.2 ambapo serikali ya kitaifa imetengewa shilingi bilioni 1,093.9 . serikali za kaunti zimetengewa A�shilingi bilioni 280.3 huku hazina ya usawazishaji ikitengewa A�shilingi bilioni 6. Kati ya mapato yote A�yaliotengewa A�serikali ya kitaifa , pesa zilizotengwa A�za misaada kwa serikali za kaunti ni shilingi bilioni A�21.9. Kwa upande mwingine A�sheria ya ugavi wa mapato iliyotiwa saini inaidhinisha kutolewa kwa shilingi bilioni A�35.6 kutoka hazina kuu. Pesa hizo zitatumiwa A�na serikali kutekeleza majukumu yake ya kifedha katika kipindi kilichosalia cha bajeti kinachokamilika tarehe 30 mwezi Juni .Rais Kenyatta pia alitia saini kuwa sheria mswada wa mabadiliko ya hali ya hewa wa mwaka 2014. Miswada hiyo iliwasilishwa A�kwa rais leo asubuhi na spika wa A�bunge la taifa A�Justin Muturi.